Mark 10:46-51

46 aKisha wakafika Yeriko. Isa alipokuwa akiondoka mjini na wanafunzi wake pamoja na umati mkubwa wa watu, kipofu mmoja, jina lake Bartimayo, mwana wa Timayo, alikuwa ameketi kando ya njia akiomba msaada. 47 bAliposikia kuwa ni Isa Al-Nasiri aliyekuwa anapita, akaanza kupaza sauti akisema, “Isa, Mwana wa Daudi, nihurumie!”

48Watu wengi wakamkemea, wakamwambia akae kimya, lakini yeye akazidi kupaza sauti, akisema, “Mwana wa Daudi, nihurumie!”

49Isa akasimama na kusema, “Mwiteni.”

Hivyo wakamwita yule mtu kipofu, wakamwambia, “Jipe moyo! Inuka, anakuita.”
50Akiwa analivua lile joho lake, alisimama na kumwendea Isa.

51 cIsa akamuuliza, “Unataka nikufanyie nini?”

Yule kipofu akajibu, “Mwalimu, nataka kuona.”

Copyright information for SwhKC